| |
Yaliyomo
Kuhusu Sisi
Miradi
Historia
Michango
Mawasiliano
|
|
Historia
You Touch Africa ni chama kipya
chakujitolea. Kamati Tendaji imeundwa na watu wenye uzoefu mkubwa
katika kukusanya fedha na vifaa kwa ajili ya Africa. Nisehemu ya
kikundi kilichokusanya fedha mwaka 2002 kwa ajili yakukarabati
Hosipitali ya Makomu Kaskazini mwa Tanzania
|
Kabla ya ukarabati, hosipitali, ilikuwa na paa lililooza,
lilivuja kila mahali, waya za umeme mbovu, na msingi ulopasuka nyufa.

Hela ilikusanywa baada ya Padre Arbo Lekule, mzaliwa wa Makomu, kuongoza kikundi cha watu watano kupanda mlima Kilimanjaro, tamasha la mziki London na jitihada nyinginezo.

Hella ilokusanywa iliwezesha kukamilisha ukarabati ulofanywa
na wenyeji wa Makomu mwaka 2003.

Baada ya kuweka paa jipya, jengo zima lilikarabatiwa na vifaa vipya kununuliwa.

Hosipitali sasa ina paa jipya, sakafu, msingi na rangi mpya, pamoja na vitanda vipya. Inahudumia wananchi wa eneo lote.

| |