![]() |
Gusa Afrika - Badili maisha |
Miradi |
||||
|
|
|
|||||
Miradi yetu ya mwanzo iko Tanzania, Afrika ya Mashariki, ambako tuna uelewa mkubwa na mawasiliano mazuri |
Paa lililopo katika Shule ya Msingi ya Makomu/Kyala limeoza kwa kutu na linalika kila mahali. Litakarabatiwa kwa awamu ili kuhakikisha kuwa watoto hawavujiwi madarasani.

Kwa sasa wanafunzi wanakula ugali au makande, kwa kadri ya mchango wao wa mahindi. Yanapokwisha wanabaki bila chakula. Tunampango wakuongeza ubora wa chakula chao kwa kununua mboga za majani, mafuta ya kupikia and matunda kutoka kwa wenyeji.
Tumekidhiwa kwamba mradi huu utanafadhiliwa na Mr Wilbert Derk Howrey LLP Amsterdam: Email:

Pale ambapo waalimu kutoka UK wamependa kwenda kufundisha huko Africa wakati wa likizo zao, tumeweza kuwapatia mawasiliano na ushauri muhimu. Lengo letu nikuwapa mwamsho wa kushirikiana kielimu, kati ya waalimu na watoto wa mashule ya Afirika na ya Ulaya..
Tumepewa msaada wa vifaa vya hosipitali na daktari wa Ulaya. Kwa sasa tunatafiti uwezekano wa kusafirisha vifaa hivyo kwenda Afrika, ili vipewe hosipitali zinazohitaji vifaa hivyo..
Tumekuwa tukishirikiana na kikundi cha Wamama Wakatoliki Tanzania (WAWATA), katika mradi wa kukopa na kulipa. Faida inayopatikana inakwenda kusaidia kulipa madeni ya wagonjwa masikini, Hosipitali ya Makomu. Tunatafiti namna ya kuupanua mradi huu.
Shule hizi ziko, zaidi ya kima cha 1900m juu ya usawa wa bahari.
Ni eneo labaridi sana la Tanzania. Kwa sasa shule hazina madirisha. Tunategemea kuwawekea madirisha.

Vibao kadhaa vimechakaa sana. Tutakarabati na kuweka vibao vyipya.